Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba imeendeleza ubabe ugenini katika michuano ya klabu bingwa Africa baada ya kuiadhibu Mbabane Swallors nyumbani kwao.

SimbaSc imeifunga mabao manne kwa sifuri Mbabane Swallors katika mchezo wa marudiano uliofanyika kwao katika uwanja wa Manzini nchini Swatziland.

Alikua ni Cletus Chota Chama aliefungua kalamu ya mabao baada ya kufunga magoli katika dakika ya 28 na 33 na kuiepeleka Simba mapumziko ikiwa inaongoza kwa mabao mawili.

Kipindi cha pili Simba ilifanikiwa kupata mabao kupitia washambuliaji wake wakigeni Emmanuel Okwi dakika ya 51 na Mesddie Kagere katika dakika  ya 63 na kuhitimisha kalamu hiyo ya mabao.

Kwa matokea hayo yanaifanya Simba kuingia katika hatua ya kwanza ya klabu bingwa Africa kwa ushindi wa jumla ya mabao 8 kwa 1.

Simba sasa inasubiri kukutana na UD Songo au Nkana Red Devil ya Zambia.

 

Sambaza....