Mabingwa Afrika

Simba wamefanikia kimalengo yao

Sambaza kwa marafiki....

Juhudi walizofanya Simba zisipuuzwe hata kidogo!..changamoto ni malengo tu!..kama ulipanga safari fupi kisha unatamani safari ndefu ukiwa uko njiani jua waliopanga safari ndefu kabla ya mwanzo wa safari watakuwa tofauti na wewe!

Nafikiri Simba mlichokifanya msimu wa CL (Ligi ya Mabingwa)  ni kutoa tahadhali kuwa maandalizi ya msimu ujao hayatokuwa sawa na msimu huu!..kiujumla mmejitendea haki!..tatizo labda litabaki pale pale kwenye kutofautisha mafanikio kwa njia ya mikakati!..kwa sababu historia pia ni shahidi unaweza ukawa bingwa mwaka huu mwakani ukatolewa round ya kwanza!..hatuweki kumbukumbu ya matamanio ya mafanikio ya zaidi ya mwaka uliopinduka!.

Wachezaji wetu huwa ni watu wa kupelekwa na mizuka na sio tamaa ya mafanikio jambo ambalo hata viongozi wetu wako hivyo hivyo!..Yanga wakiwa na hali nzuri kabisa wamepiga marktime miaka minne ni kuonesha namna gani vision na mission ya mafanikio ilivyokuwa DHAIFU!..huwa tunapelekwa na mihemuko zaidi ya mikakati!..kila la kheri ktk mikakati yenu ya nje na ndani ya uwanja ktk kumaliza viporo!

#KandandaChat, Ismail Mohammed (Akiwa China)

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.