Kikosi cha Simba kikiwa mazoezini.
Mabingwa Afrika

Simba yafanya mazoezi yake ya mwisho kabla ya kuelekea Misri.

Sambaza kwa marafiki....

Simba sc leo jioni inaelekea nchini Misri ambapo wanakwenda kumenyana na vinara wa kundi D na wababe wa Africa Al-Ahly jijini Alexandria nchini Misri katika muendelezo wa michezo ya Klabu Bingwa Africa.

Ikiutumia uwanja wa Bokko Beach Veteran uliopo Ununio Simba ilianza mazoezi hayo majira ya saa nne asubui huku yakisimamiwa vilivyo na benchi lote la ufundi la Simba sc chini ya kocha Mbelgiji Patrick Aussems.

Kama kawaida walianza kwa sala a kuongea kidogo kwa muda wa dakika 5 kisha wakaanza wakaanza kukimbia kwa kuzunguka uwanja. Mazoezi hayo yalisimamiwa na kocha Mtunisia wa viungo kwa umakini mkubwa. Baada ya kukimbia kwa robo saa kocha wa viungo alipanga koni na kuwataka kukaa wawili wawili huku wakinyoosha viungo na kuchezea mpira.

Upande wa mwingine kocha wa makipa wa Simba sc Muharami Mohamed yeye alikua akkwafua vilivyo makipa wake watatu Ally Salim, Deo Dida na Aishi Manula. Baada ya dakika 10 wote walikua wamemaliza na kocha mkuu kugawa vikosi viwili ili kucheza “full game” huku akiukata uwanja na kutumia mita 70 kwa kutumia koni.

Vikosi vilivyokua:

Kikosi cha kwanza kilikua na Manula, Mzamiru, Bukaba, Mlipili, Tshabalala, Vitaly, Niyonzima, Mo Ibra, Kichuya, Salamba Abdul Selemani na

Kikosi cha pili kilikua na Dida, Gyan, Kwasi, Juuko, Wawa, Kotei, Dilunga, Rashidi, Okwi, Kagere.

Kiungo mpya hatari

Simba sc imeshusha kiungo mpya kutoka Ivory Coast ili afanye majaribio ambapo tangu siku ya Jumamosi amekua na kikosi hicho. Katika mazoezi ya leo ameonekana akizingatia kwa hali ya juu maelekezo yote aliyokua akipewa na mwalimu.

Alipofika alianza kwa kuzunguka uwanja huku akikimbia na mpira raundi 5 huku akisubiri mazoezi ya jumla ya timu. Hata katika mazoezi ya viungo alionekana kuyamudu vizuri. Hata walipoanza walipocheza full game Vitally alionekana ni kiungo mwenye utulivu wa hali ya juu huku akicheza katika nafasi “zone” yake bila kutoka. Lakini pia ameonyesha uwezo mkubwa wa kupiga pasi ndefu na fupi.

Mkude achelewa akiona cha moto.

Jonas Mkude alifika mazoezini hapo akiwa amechelewa zaidi ya sa moja na hivyo kuwakuta wenzake wanaendelea na program za mwalimu. Alipokelewa na mwalimu wa viungo na kuaza kumuheshenyesha katika koni.

Alipangiwa koni na kupewa mazoezi mpaka pale wenzake walipomaliza program zote za mazoezi kwa ujumla.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.