Mabingwa Afrika

Simba yamkwepa bingwa mtetezi, yarudi teña Congo

Sambaza kwa marafiki....

Wawakilishi Tanzania katika michuano  ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Simba imepangwa kucheza na TP Mazembe katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

 

Simba imewakwepa mabingwa watetezi Esparance ya nchini Tunisia. Esparance  imepangiwa kucheza na FC Constantine. Sumba itaenda Congo kwa Mara ya pili baada ya kwenda kwenye hatua ya makundi msimu huu dhidi As Vita walipofungwa goli 5-0.

Mshindi wa kwanza wa kundi alilokuwepo Simba, Al Alhly ya Misri imepangwa kucheza na Mamelod Sundows ya nchini Afrika Kusini. Wydad imepangwa kucheza na Horoya ya Guinea. Simba itaanzia ugenini dhidi TP Mazembe.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.