Kombe la Dunia

Tanzania yafuzu kombe la dunia!

Sambaza....

Timu ya soka ya Taifa ya wanawake walio chini ya miaka 17 “Serengeti Girls” wamefanikiwa kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia la umri wao baada ya kuiondosha Cameroon.

Serengeti Girls wamefanikiwa kuifunga Cameroon kwa ushindi wa jumla wa mabao matano kwa moja baada kupata ushindi wa mabao manne kwa moja ugenini na kushinda bao moja bila nyumbani katika mchezo uliopigwa uwanja wa Aman Zanzibar.

Mchezaji wa Serengeti Girls akiwatoka wachezaji wa Cameroon.

Hii ni kwa mara ya kwanza Tanzania inafanikiwa kupata ushindi na kufuzu katika michuano ya kombe la Dunia katika mchezo wa soka.

Timu hiyo iliyo chini ya kocha “Mchawi Mweusi” Bakari Shime akisaidiwa na Edna Lema “Mourinho” imefanikiwa kufika hatua hiyo baada ya kuiondosha Burundi pia katika hatua za awali.

Edna Lema akishangilia na wachezaji wake baada ya mchezo kumalizika.

Hongera Serengeti Girls, Hongera na wote walifanikisha Tanzania kuandika historia mpya katika soka.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.