Ligi

Tariq Seif atumia mechi moja tu kumfikia Kagere !

Sambaza....

Jana kulikuwa na mechi kati ya Yanga na Biashara United katika uwanja wa Taifa , mechi ambayo tulishuhudia ikimalizika kwa Yanga kushinda goli 1-0 , goli lililofungwa dakika 84 na mchezaji wa zamani wa Biashara United ambaye kwa sasa anacheza Yanga Tariq Seif.

Mtandao wa Kandanda . Co. Tz huwa unatoa kiatu kwa kushirikiana na Mgahawa Cafe kwa mchezaji ambaye anafunga magoli mengi kwa mwezi. Kila mwezi huwa anapatikana mchezaji ambaye hupewa kiatu kama mfungaji bora wa mwezi husika, mpaka sasa hivi

Meddie Kagere ndiye aliyepewa kiatu hicho na Kandanda.Co.tz , kwa mwezi huu wa kumi na mbili Meddie Kagere inaonekana kasi yake imepungua sana , ana goli moja katika mechi mbili alizocheza za ligi

Tariq Seif ametumia mechi moja tu kumfikia kwenye orodha ya wafungaji bora wa mwezi wa kumi na mbili ambapo mshindi hupewa kiatu na Kandanda. Co.tz


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.