Masau Bwire msemaji wa Ruvu Shooting
Blog

Timu yetu haina njaa, ni zaidi ya Rollers na Zesco-Masau Bwire

Sambaza kwa marafiki....

Baada ya Ruvu Shooting kufanikiwa kupata ushindi dhidi ya Yanga katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom amedai kuwa msimu huu wanaweza wakawa mabingwa.

Akizungumzia kuhusu waamuzi wa mchezo huo, amedai kuwa kama waamuzi wakifuata sheria zote Ruvu Shooting itakuwa bingwa.

“Wakati ligi inaanza, mwenyekiti wa kamati ya waamuzi, Salum Chama alidai mwamuzi yoyote ambaye atakataa goli au kutoa goli ambalo siyo halali basi akalime mpunga”

” Nawaomba kamati ya waamuzi waliangalie lile goli lililokataliwa kama watakuta ni goli halali basi wafanye walichokisema”.

Akizungumzia kuhusu uwezo wa Ruvu Shooting msimu huu amedai kuwa wana nafasi ya kubeba ubingwa.

“Kama waamuzi watachezesha vizuri kwa maandalizi tuliyoyafanya lazima tubebe ubingwa hakuna wa kutuzuia”.Alipoulizwa kuhusu uwepo wa kocha mpya wa Ruvu Shooting , Salum Mayanga amedai kuwa wamepata kocha bora.

” Tumepata kocha bora anayejua mpira, anayejua kusoma mpira vizuri ndiyo maana Leo tumewafunga Yanga”

Kuhusu Papasa Squared amedai msimu huu imeboreshwa sana kuliko ya msimu Jana

“Msimu jana tuliona ile Papasa Squared iliyokuwa chini ya NOTO ikilegea, lakini nawahakikishia msimu huu tutawapapasa ipasavyo msimu huu”.

” Tutahakikisha tunapapasa mpaka mtu akizeeka akiwa amezeeka na wajukuu zake awasilimulie kuwa kulikuwepo na Ruvu Shooting ”

Kuhusu uwezo wa wachezaji wa Ruvu Shooting , Masau Bwire ameomba Ruvu Shooting kupata nafasi ya kuliwakilisha taifa kimataifa.

“Ruvu Shooting ina wachezaji wa Tanzania. Wanaojituma, kwa hiyo wanatakiwa kupewa nafasi kwa ajili ya kuliwakilisha taifa letu”.

Sisi ni zaidi ya Town Ship Rollers , Zesco. Tunavyocheza kama kungekuwa na nafasi ya kubadilisha timu ya kutuwakilisha kimataifa tungepelekwa sisi, kwanza sisi hatuna njaa”- alimalizia Masau Bwire

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.