Blog

Tutaanza ligi na mdhamini – Wambura

Sambaza kwa marafiki....

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi kuu bwana Boniface Wambura amedai kuwa mdhamini wa ligi kuu ameshapatikana mpaka sasa hivi.

“Mdhamini ashapatikana tayari, muda huu , asubuhi hii ndiyo nataoka kwenye kikao cha kujadiliana kuhusu mambo ya mkataba wa mdhamini huyo wa ligi kuu”

Alipoulizwa na mtandao huu kuhusu uwezekano wa kuanza ligi kuu na mdhamini amedai kuwa huo uwezekano upo kabisa.

“Tutaanza ligi tukiwa tumeshamtambua mdhamini huyo, na hapa tupo kwenye taratibu za mwisho za kumpata ndiyo maana tumetoka kwenye kikao cha kujadili mambo ya mkataba asubuhi hii ya leo”- alidai mtendaji huyo mkuu wa bodi ya ligi kuu.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.