Sambaza....

Mchezaji wa zamani wa Chelsea Tony Cascarino amemshauri kocha mpya wa Arsenal Unai Emery kuwaondoa wachezaji nane kikosini akiwemo mshambuliaji wa Mnigeria Alex Iwobi.

Cascarino anaamini kwamba mchezaji Iwobi mwenye umri wa miaka 22 hawezi kuimarika zaidi ya kiwango chake cha sasa na anatakiwa kuondolewa kikosini.
“Sidhani kama Iwobi anaweza kuwa mchezaji wa kiwango cha kuu zaidi ya hapo alipofikia kama vile Arsenal wanavyohitaji wachezaji wa aina hiyo kwa sasa,” Cascarino ameiambia jarida la Times la Uingereza.

Iwobi ambaye ataiwakilisha nchi yake katika michuano ya kombe la mwezi ujao nchini Russia, ameichezea Arsenal michezo 39 akifunga mabao matatu pekee yake na kusaidia kupatikana kwa mabao 7 msimu huu.

Mbali na Iwobi wachezaji wengine ambao ameshauri waondolewe kikosini ni pamoja na Hector Bellerin, Petr Cech, Shkodran Mustafi, Laurent Koscielny, Calum Chambers, Granit Xhaka, Aaron Ramsey na kiungo Mesut Ozil.

Sambaza....