Sambaza....

Mwanariadha mstaafu Usain Bolt ameiaga klabu ya Central Coast Mariners baada ya kumaliza mazoezi ya kujiunga na timu hiyo ya nchini Australia bila ya kufuzu.

Mjamaika huyo mwenye umri wa miaka 32, mshindi wa medali za olimpiki mara 8 mfululizo kwenye mashindano ya kusprint,Alijiunga na klabu hiyo August mwaka huu ‘kwa mazoezi yasiyokuwa na muda rasmi’ katika ligi ya Australia.Alibahatika kufunga magoli 2  katika jitihada zake za kwanza katika mchezo wa kirafiki,lakini hakucheza mechi hata moja ligi ilipoanza .

Mmiliki wa klabu hiyo Mike Charlesworth amemshukuru Bolt kwa majaribio yake ya wiki 8,akiyaelezea kuwa na mafanikio makubwa.

Mike alisema,‘ameshirikiana vizuri  na Wachezaji wenzake na kuonyesha umahili mkubwa sana kama mchezaji kwa kipindi chote alichokuwa nasi ’.

Usain Bolt

‘Tukiachana na kutofikia makubaliano ambayo yange endeleza safari ya kisoka ya Usain Bolt katika klabu hii,tumefurahia sana kuwa na mshindi wa dunia wa mbio za olimpiki kwa wiki hizi 8,’Aliongezea Mike.

Bolt anashikilia rekodi ya Dunia ya kukimbia Mita 100 na 200.Pia Bolt amesema ndoto yake kubwa ni kucheza Soka la kulipwa kama walivyo wachezaji wengine wanaotamba kwenye ulimwengu wa soka na kuwa kwenye Historia nyingine ya kimichezo ukiachilia mbali historia kubwa aliyoiacha kwenye mchezo wa Riadha.

Licha ya kutupwa nje ya kikosi cha Central coast Mariners Bolt alisema  ‘Napenda kuwashukuru wamiliki wa Central Coast Mariners,uongozi,staff,wachezaji wenzangu na mashabiki kwa ujumla kwa kunifanya nijisikie nipo nyumbani kwa heshima na ushirikiano mulionionyesha, nimejifunza mengi kutoka kwenu na nachukuwa hii kama mwanzo wa maisha yangu mapya huko niendako  nawashukuru sana na nawapenda wote,’Alisema Bolt.

Bolt alistaafu riadha mwaka 2017,alishawahi kufanya majaribio na timu ya Borussia Dortmund,klabu ya Afrika kusini Mamelodi Sundowns na klabu ya Stromsgodset.

-Imeaandaliwa na Lodrick Sindi


Sambaza....