Mataifa Afrika U17

Wachezaji watano hatari AFCON -U17

Sambaza kwa marafiki....

Michuano ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 Afrika, Afcon inaanza jumapili hii. Hii itakuwa michuano ya 13 tangu kuanza kwake. Ni michuano ambayo hutoa vipaji vingi. Hivi hapa ni vipaji vitano ambavyo vinaonekana ni bora na hatari katika michuano hii.

THOMAS KAKAIRE-UGANDA

Hapana shaka huyu akitajwa ƙkitu kinachokuja kwenye akili za wengi ni michuano ya vijana waliochini ya umri wa miaka 17 kanda ya CECAFA iliyofanyika hapa Tanzania. Anacheza kama mshambuliaji wa pili, pia anacheza kama mchezeshaji (playmaker). Alifanikiwa kufunga magoli 3 katika michuano hiyo na alikuwa mhimili mkubwa sana na timu yake ya Uganda katika michuano hii.

Thomas Kakaire

ZITO LUVUMBO-ANGOLA

Tunapozungumzia umuhimu wa vituo vya kulea, kukuza vipaji ndipo hapa unapokuja kupata watu kama hawa kina Zito Luvumbo.

Katoka kwenye kituo cha Angola’s Primeiro De Agosto. Huyu ndiye alikuwa mchezaji bora wa michuano ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 kanda ya COSAFA huku akifunga goli 3 na kuisaidia timu yake kubeba ubingwa mbele ya Tanzania kwenye fainali. Mpaka sasa klabu ya Manchester United imeonesha nia ya ƙkumtaka mchezaji huyu.

Zito LUVUMBO

JOHN EDMUND-TANZANIA

Wengi tulikuwa hatumjui, kaja kutushitua kwa kile alichokifanya Rwanda akifunga magoli 3 ndani ya mechi mbili.

Baada ya Kelvin John kuumia tulipatwa na hofu nani anaweza kutubeba , ghafla akaja John Edmund tena akaja akiwa na moto mkali. Ana kipaji kikubwa sana,anajua kukaa eneo sahihi ndani ya uwanja, anaju kufunga na kutoa pasi za mwisho. Huyu ni mchezaji mwingine ambaye anaangaliwa kwa uzito mkubwa katika michuano hii.

LIONEL WAMBA-CAMEROON

Moja ya wachezaji ambao wanaangaliwa sana na vilabu vingi barani ulaya kwa sasa. Mshambuliaji hatari wa kati ambaye anauwezo wa kufunga, kumiliki mpira na kutoa pasi ya mwisho ya goli.

Kelvin John akipongezwa na wenzake

KELVIN JOHN

Utaandikaje orodha hii bila ƙkumtaja Kelvin John “Golden Boy”. Mfungaji bora na mchezaji bora wa michuano ya Afcon 17 kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA?

Huyu ndiye moyo wa timu yetu ya taifa ya vijana waliochini ya miaka 17 Serengeti Boys. Ndiyo maana alipoumia Rwanda tulipata hofu lakini kwa sasa yuko fit kwa mapambano. Ni mchezaji ambaye anatazamiwa kuwa hatari zaidi katika michuano hii ya CECAFA

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.