EPL

Wachezaji watano waliombeba Arteta jana dhidi ya Manchester United

Sambaza....

 

Jana Mikel Arteta alipata ushindi wake wa kwanza tangu aichukue Arsenal kama kocha mkuu. Mechi yake ya kwanza ya mashindano ilikuwa dhidi ya AFC Bournamouth alitoka sare kisha akafungwa na Chelsea na jana akashinda dhidi ya Manchester United. Wafuatao ni wachezaji watano waliombeba jana.

LACAZETTE

Inawezekana kwenye mechi zote ambazo amecheza chini ya Mikel Arteta hajafanikiwa kufunga hata goli moja, lakini jana alifanya kazi kubwa , alikuwa na uwezo wa kukaba juu , kushuka chini kusaidia kiungo , kuwafanya mabeki wa Manchester United wawe na kazi moja ya kupambana naye na alikuwa beki wa kwanza wa Arsenal.

PEPE

Swali kubwa ni lini ataonesha kiwango cha bei aliyonunuliwa ya Euro 72 M? Chini ya Unai Emery hakuwa na kiwango kikubwa sana . Jana alionesha thamani yake , alifunga goli , na alikosa goli ambalo liligonga mwanga , huyu alionesha ukomavu wa hali ya juu.

 

OZIL

Huyu hakuwa na maelewano mazuri na kocha aliyepita Unai Emery , aliwekwa benchi . Lakini tangu aondoke Unai Emery na Mikel Arteta kuja Arsenal , Mesut Ozil amekuwa mkomavu . Siyo Mesut Ozil mzembe ambaye watu wengi walikuwa wanamssma , ana kaba jana ndiye mchezaji aliyekimbia umbali mrefu mbele ya Fred na Torreira.

DAVID LUIZ

Huyu alisemwa ni garasa lakini jana alionesha ukomavu wa hali ya juu. Timu inacheza ikitokea nyuma. Anapiga pasi ndefu vizuri anakaba vizuri na anawaongoza wenzake vizuri.

TORREIRA

Huyu ndiye mwenye Arsenal yake. Chini ya Unai Emery huyu alitaka kurudi zake ligi kuu ya Italy Serie A Baada ya kuonekana kutopata nafasi sana. Lakini Mikel Arteta kamfufua , jana kakimbia umbali mrefu nyuma ya Ozil na Fred , kakimbia kilomita 11.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.