Mabingwa Afrika

Wanaokwenda Misri hawa hapa, nahodha hayumo.

Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba sc leo jioni inaelekea nchini Misri tayari kabisa kuwakabili wenyeji wao Al-Ahly katika mchezo wa tatu wa Ligi ya Mabingwa wa kundi D.

Simba sc inaelekea Misri huku ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao matano ugenini kutoka kwa AS Vita. Mwalimu Patrick ametaja orodha ya majina 20 ya wachezaji watakaoelekea nchini Misri huku jina la nahodha John Bocco likikosekana.

John Bocco annakosekana katika msafara huo kutokana na majeruhi aliyoyapata katika mchezo wa kwanza wa Simba dhidi ya JS Souara katika uwanja wa Taifa.

Kikosi kinachokwenda Misri;

Aishi Manula, Deo munishi, Mohamed HusseinAsante kwasi, Pascal wawa, Juuko Murushed, Paul Bukaba, Nicholaus Gyan, James kotei, Jonas Mkude, Haruna Niyonzima, Mdhamiru Yasin, Hassan Dilunga, Mohamed Ibrahim, Shiza kichuya, Juma Rashidi, Emmanuel Okwi, Meddie Kagere, Adam Salamba, Cleotus Chamma.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.