Aliyewahi kuwa kocha wa Arsenal kwa muda wa miaka 22 mfululizo, Arsene Wenger Leo hii ameweka wazi kuwa atarudi rasmi mwezi wa kwanza mwaka 2019.
Arsene Wenger mpaka sasa hajaweka wazi kuwa atarudi kama nani kwenye tasnia hii ya mpira. Kuna habari nyingi ambazo zinamhusisha kocha huyu aliyepata mafanikio makubwa akiwa na Arsenal.
Timu ya taifa ya Japan inahusishwa kutaka kumchukua awe kocha mkuu wa timu ya taifa ya Japan. Huku Japan ikiamini kabisa kuwa Arsene Wenger anaujua utaratibu wa soka la Japan kwa sababu ameshawahi kufundisha soka nchini humo.
Wakati huo huo Klabu ya PSG ya Ufaransa inahusishwa pia kumchukua kocha huyu mkongwe awe mmoja ya watu ambao watakuwa wanahusika na mambo ya usajili wa klabu hiyo.
Wakati PSG wakiripotiwa kumtaka, kuna habari zinazodai kuwa klabu ya Manchester United inamtaka kocha huyu kama mbadala wa kocha wa sasa Jose Mourinho.
Arsene Wenger amedai kuwa mpaka sasa akili yake imeshapumzika vya kutosha na anaona kabisa huu ni wakati mzuri na sahihi kabisa kwake yeye kurudi kwenye kazi yake ya mpira wa miguu.