Stori

Yanga wamempata Didier wao? – 2

Sambaza....

Wapwa huu ni muendelezo wa matukio ya kiufundi katika mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Aigle Noir uliopigwa katika kilele cha siku ya Mwananchi.

Naamini Tuisila akizoeana kiuchezaji                   (combination) yake na Mustapha ule upande unaweza kuwa na faida au ikawa (strong part )ya Yanga hasa Tuisila akikumbuka kumtandikia Reli Mustapha wakati wa kupanda kuongeza kushambuli apite kiwepesi kuna muda waliikuwa wanagongana kwa kuwa Tuisila anakaa njiani had deep ndani.

Michael Sarpong real strike mwenye uchu na kiu ya hali ya juu dk 5 za mwanzo alikuwa amesha jaribu kupiga golini kwa mpinzani mara mbili moja ilikuwa kwa mguu na ya pili ilikuwa ya kichwa. Kwa uchu ule akajikuta anatoka kwenda kutafuta mipira nje ya box kama timu itazoeana na walimu kuliona hili wanaweza kumpunguzia eneo la kucheza akawa na faida zaidi kwa timu.

Michael Sarpong.

Kuna wakati alionesha element za akina Drogba kureceive mpira wa juu toka goli kick huku akiruka na mabeki wawili “akaunywa” kifuani lakini opponent wakamsukuma kwangu ilinipa sign kuwa ni Pure striker hadi mapumziko alikuwa amelijaribu lango mara nne. Kwa mchezaji wa position yake ni mzuri na niligundua amejaliwa vitu viwili ni Player maker lakini pia ni fighter.

Anajua kutumia ukubwa wa umbo lake na anaakili sana ya mchezo angalia goli lake la kichwa anacommand (chagua)sehemu ambayo anahuakika kipa hawezi rudi tena kule kwa kuwa alitokea kule kifupi analeta matumaini sana kwamba” ana kitu.

Carlinhos nianze kwa kusema anakipaji kikubwa kama mchezaji anaakili sana ya mchezo alicheza dakika nchini ya kumi lakini alifanya vitu vichache kwa faida ya timu ,naye ni muhanga wa atmosphere ya uwanja kwa jana mpira wake wa kwanza alianza kwa kuukosena.

Carlinhos.

Makocha wa zamani wanasema alipima raizon au mguu umetoboka alitaka kuutuliza ukampita lakini kitu kizuri nyuma yake kulikuwa na mchezaji nwenzie wa timu yake lakini alikuja kufanya vitu viwili vya kimpira vilitosha kujua uwezo wake.

Kwanza alibadilisha mpira mmoja toka pande moja kwenda mwingine kwa umbali wa mita 25-30 kwa kimo cha Ng’ombe kabla ya kuja kupiga shuti zito muda fulani wa mchezo, anaashiria anakipaji japo kwa football yetu anahitaji kuongeza nguvu au jihadi si mpambanaji (fight) ni softicated Player ambao huwa wanajengwa na ufundi mkubwa, nitamuangalia kwa nafasi nyingine tena.

 

Ditram Nchimbi

Ditram Nchimbi “Duma” na Deus Kaseke (nahodha wa mchezo) good performance toka kwao kama kawaida  ni wapambanaji wazuri.

Sambaza....