Blog

YANGA yala matapishi yake!, yamrudisha NIYONZIMA

Sambaza....

Baada ya kuondoka na kwenda upande wa pili , upande ni wa upinzani mkubwa kwa Yanga,  yani upande wa Simba, klabu ya Yanga inaonekana kumrudisha tena Haruna Niyonzima katika kikosi chake.

Amekaa nje ya Yanga kwa kipindi cha miaka mitatu ,na awali alionekana ni kipenzi kikubwa cha mashabiki wa Yanga kutokana na uwezo wake mkubwa ndani ya uwanja.

Niyonzima wakati wa mchezo wa Samatta vs Alikiba

Haruna Niyonzima anayesajiliwa moja kwa moja kutoka katika klabu ya FC Kigali ya nchini Rwanda inaonesha kwa asilimia kubwa anarudi Yanga sehemu ambayo inaonekana kwake ni Nyumbani.

Kwa mujibu wa Habari za ndani ya klabu hiyo kesho Haruna Niyonzima atatambulishwa rasmi kama mchezaji halali wa Klabu ya Yanga. Yanga inajiandaa vilivyo na mechi za ligi kuu ikiwemo mechi ya Simba itakayochezwa tarehe 04/01/2020.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.