Ligi Kuu

Achaneni na habari za uongo-PATRICK AUSSEMS

Sambaza....

Kuna maneno mengi sana ambayo yanazungumzwa mtaani kuhusu kocha wa Simba na hatima yake ndani ya klabu ya Simba. Mengi yanasemwa kuwa mechi ya Jana ndiyo ilikuwa mechi yake ya mwisho akiwa na Simba.

Baada ya ushindi wa jana wa magoli matatu kwa bila (3-0) dhidi ya Ruvu Shooting kocha huyo kupitia ukurasa wake wa instagram amewapongeza wachezaji wake kwa kucheza kwa weledi na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0 bila kujalisha maneno ya uongo yanayoongewa nje.

Kwa mantiki hii kinachoonekana ndani ya Simba ambacho kinasikika sana nje ni cha uongo kwa mujibu wa kocha huyo mkuu, na hakuna ukweli wowote wa kile kinachoongolewa kuwa mechi ya Jana ndiyo ilikuwa mechi yake ya mwisho akiwa na timu ya Simba.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.