Mataifa Afrika

Algeria wababe lakini kwa Mkapa hatoki mtu!

Sambaza....

Ni ukweli usiyofichika kwamba Algeria ametuzidi kwa mengi kwenye soka kuanzia uwezo wa mchezaji moja moja na mafanikio timu kiujumla hasa tunapokuja kwenye level ya timu za Taifa.

Wenzetu wamekuwa wakishiriki Kombe la Dunia tangu zama hizo akianza kwa mara ya kwanza mwaka 1982 wakiwa na nyota kibao akina Rabah Madjer.

Tangu hapo wamejenga tamaduni ya kushiriki mara kwa mara michuano mikubwa mbalimbali inayohusisha timu za Taifa na si tu kuwa washiriki bali kwenda kuwa washindani wa kweli hasa kwenye michuano ya AFCON.

Kikosi cha Algeria kilichotwaa kombe la Afcon mwaka 2019.

Tunapowania nao tiketi ya kwenda kushiriki kwa mara ya tatu tangu kombe hili limeanzishwa mwaka 1956 wao wamepata kushiriki mara 19 na kutwaa ubingwa mara mbilia 1990 na 2019 nadhani hadi hapo unaona utofauti wetu.

Kule ambako sisi hatujafanikiwa kutoboa            (kombe la Dunia) wao wameshiriki mara 4 kwenye soko la wachezaji Ulaya wao wana wachezaji wengi mno karibu kila ligi na wakicheza kwa mafanikio kama nahodha wao wa sasa Riyad Mahrez ambaye bahati nzuri hajaja na timu katika huu.

Lakini kuna namba hatari ambazo zimekuja na zikiwa zimetoka kwenye mafanikio ya ligi zao huko Ulaya Islam Sliman akitokea Sporting CP ambapo amemaliza akiwa na msimu mzuri na ndiyo mfungaji bora wa muda wote katika timu ya Taifa akiwa amefunga magoli 40 katika michezo 86 zikiwemo goli tano alizotufunga sisi Watanzania tangu mwaka 2015 alipocheza kwa mara ya kwanza nasi.

Mshambuliaji wa Stars Adi Yusuph alipiga mpira mbele ya mlinzi wa Algeria.

Algeria ni kama wamefanya mapinduzi makubwa kwenye miaka hii ya karibuni awali ya yote tulikuwa tunatoshana nguvu kweli kwenye mechi zetu zipo tulizopata ushindi sisi na wapo walioshinda wao tangu 1973 tulipokutana kwa mara ya kwanza.

Tumecheza jumla ya michezo 11 na huu unaenda kuwa wa 12 tumeshinda moja mwaka 1995 hapa Dar-es-Salama kwa magoli ya Madaraka Seleman na Juma Bakari ‘Kidishi ‘ lakini tumewahi kupata sare 4 zikiwemo kule 2 kule kwao nyakati hizo ila kuanzia 2015 kwenye ‘generation ‘ yao ya sasa mambo yamekuwa magumu kwetu katika michezo
katika michezo 4 ya mwisho kukutana nao tumepata sare moja ya 2-2 Dar-es-salaam nakuchezea vichapo vikubwa vilivyofanya tuwe tumefungwa jumla ya goli 16.

Farid Mussa akifunga bao mbele ya mlinda mlango wa Algeria.

Ugeni wakati wa kwenda si wakati wa kurudi, tuna nafasi ya kufanya vizuri dhidi yao kwa kupata matokeo mazuri kuanzia leo Estadio De Mkapa.

Moja ya siri kubwa inayiwapa ushindi mara kwa mara ni “exposure” ya wachezaji wao wanaocheza Ulaya kama akina Yocef Belaili anyecheza Stade Brestois France, Rachid Ghazzal Besiktas Uturuki, Ismael Bennecer AC Milan top Golie Rais M’bolhi.

Angalau na sasa nasi tuna wachezaji kadhaa wanaocheza nje tofauti na tulivyokutana 2015 vijana wadogo damu changa kama Novatus Dismas Kelvin John, Ben Stakie, Haji Mnoga na wengineo wakibadilishana uzoefu na nahodha Mbwana Samatta pamoja na Simon Msuva naamini hatuwezi kupoteza point zote 3.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.