Mataifa Afrika

Beki Simba kuukosa mchezo wa kesho.

Sambaza....

Nyota wa zamani wa klabu ya Simba na timu ya Taifa ya Uganda “The cranes” ataukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kesho kati ya Simba Sc na Vipers katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Juuko Mursheed ambae kwasasa anaitumikia Vipers ya kwao Uganda anakosekana katika mchezo huo wa kesho kama ambavyo aliukosa ule uliopigwa katika Dimba la St Mary kwao Uganda.

 

Juuko anaungana na nahodha Milton Kalisa na majeruhi wa muda mrefu Marvin Youngman ambao pia wataukosa mchezo huo wa marudiano.

Mlinzi huyo wa kati alikuwepo wakati Simba inafuzu robo fainali mbele ya AS Vita katika msimu wa mwaka 2019 kabla yakutolewa na TP Mazembe robo fainali.

Juuko Mursheed

Kikosi kamili cha Vipers kitakachotua nchini kucheza dhidi ya Simba:

Makipa: Alfred Mudekereza, Fabien Mutombora.

Walinzi: Livingstone Mulondo, Hilary Mukundane, Isa Mubiru, Ashraf Mandela, Bashir Asiku, Enock Luyima.

Viungo: Abdu Lumala, Siraje Sentamu, Olivier Osomba, Robert Serge Mwenge, Abdu Karim Watambala, Najib Yiga, Frank ‘Zaga’ Tumwesigye.

Washambuliaji: Ibrahim Orit, Martin Kizza, Yunus Sentamu, Abubakar Lawal, Israel Desire Tety

Sambaza....