Sambaza....

Uongozi wa Klabu ya soka ya Alliance ya Jijini Mwanza umekanusha taarifa zilizoanza kuenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa timu yao imesambaratika kwa zaidi ya wachezaji sita kuondoka kambini.

Akizungumza na mtandao huu Afisa Habari wa Alliance Jackson Luka Mwafulango amesema taarifa hizo zimelenga kuwaondoa mchezoni kipindi ambacho wanajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Singida United Jumamosi hii.

“Naomba nitumie mtandao wako kukanusha hili, hakuna taarifa yoyote ya wachezaji sita kuondoka kambini na Watu wasitumie kama mind game kuelekea katika mchezo wa kesho,” amesema.

Alliance ambayo ndiyo inashika mkia kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara wakina na alama nane Jumamosi hii saa 10:00 jioni watajitupa uwanjani kuumana na Singida United kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Sambaza....