Blog

Mashabiki wa Yanga wananipenda -Mwinyi Zahera

Sambaza....

Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga , Mwinyi Zahera amedai kuwa asilimia kubwa ya mashabiki wa Yanga wanampenda kwa kiasi kikubwa.

Akizungumza na kipindi cha mshikemshike cha Azam TV , Mwinyi Zahera amedai kuwa ukiwauliza mashabiki 100 wa Yanga basi mashabiki 98 wanampenda Mwinyi Zahera.

“Mashabiki wa Yanga wananipenda mpaka kufa. Ukizungumza na mashabiki 100 wa Yanga basi mashabiki 97 au 98 basi wananipenda sana” – alisema Mwinyi Zahera.

Mwinyi Zahera amedai kuwa kuna baadhi ya mashabiki wa Yanga wachache ambao walitumwa ili waje kumtukana yeye.

“Ni mashabiki wachache tu ambao hawanipenda. Ukiangalia kuna mashabiki walitumwa kuja kunitukana lakini baadaye walikuja kuniomba msamaha”-alimalizia Mwinyi Zahera.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.