Blog

Arsenal kupoteza washambuliaji wake wote?

Sambaza....

Kuelekea kufunguliwa kwa  dirisha kubwa la usajili ambalo kwa kiasi kikubwa litaathiriwa na mlipuko wa ugonjwa wa corona tayari klabu ya Arsenal ipo katika wakati mgumu wa kuwazuia nyota wake wa safu ya ushambuliaji.

Safu ya ushambuliaji ya Arsenal inaongozwa na nahodha kutoka Gabon Pierre Emerick Aubameyang na mshambuliaji kutoka Ufaransa na nyota wa zamani wa Olyimpic Lyon Alexander Laccazate.

Pierre Emerick Aubameyang.

Aubameyang amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake huku vilabu mbalimbali vya Ulaya vilitajwa kuitaka saini yake kwa udi na uvumba. Baadhi ya vilabu hivyo ni pamoja na PSG, Real Madrid na majirani zao Manchestar United ambao wanataka kurudia nyakati za Robin Van Persie. Kutokana na muda wa mkataba wake Arsenal itahitaji kiasi kisichopungua pauni milioni 20 ili kumuuza nyota huyo.

Kwa upande wa Laccazate anawaniwa na Inter Milan ili aende kuziba nafasi ya Muargentina Lautaro Martinez ambae amekua na msimu mzuri hivyo vilabu vikubwa Ulaya (Real Madrid na Barcelona) vimemfungia kazi na kutaka kumng’oa Italia. Pia Athletico Madrid wanamtaka Laccazate kama mbadala wa Diego Costa na kocha wa ATM Diego Simione huenda akamtumia winga Thomas Lemar kama chanmbo kwa Arsenal ili kumpata Mfaransa huyo.

Alexander Laccazete

Wawili hao kwa pamoja wameifungia Arsenal mabao 24 Laccazete (7) na Aubameyang (17) huku akiwa juu ya msimamo wa wafungaji bora sawa na Jimmie Vardy wa Leicester city.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.