Tetesi

Arsenal mbioni kumshusha Kluivet.

Sambaza....

Klabu ya soka ya Arsenal imeonyesha kupendezwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa AS Roma Justin Kluivert ikiwa ni sehemu ya mpango mpya wa kocha Mikel Arteta ya kukisuka kikosi chake upya.

Arsenal wanataka kumtumia kiungo wake raia wa Armenia Henrikh Mkhitaryan katika uhamisho huo ambapo mchezaji huyo atahamia nchini Italia jumlajumla baada ya sasa kuitumikia AS Roma kwa mkopo.

Kulingana na ripoti nchini Italia Arsenal wana mpango wa kubadilishana nyota hao wawili ambapo Arsenal na Roma wanaweza kukubaliana kwa masharti, ripoti ya Gazzetta Dello Sport inathibitisha.

Mtoto huyo wa nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Uholanzi na Barcelona Patrick Kluivet  hapo awali alikuwa akihusishwa na kuhamia katika  Ligi Kuu Uingereza  kabla ya kuondoka Ajax na kutimkia AS Roma mwaka 2018, wakati Mkhitaryan ameonyesha hamu yake ya kuondoka Arsenal na kujiunga na Roma kabisa mazima.  kulingana na ripoti nchini Italia.

Mpaka sasa Justine Kluivet ameifungia mabao mabao saba AS Roma msimu huu akitoa na pasi moja ya bao. Arsenal haina uhakika na washambuliaji wake wawili (Aubameyanga na Laccazate) kama watasalia msimu ujao hivyo wameanza mapema kutafuta mbadala wao.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.