Ligi Kuu

Azam Fc wakubali yaishe waache wataalam wafanye kazi!

Sambaza....

Klabu ya Azam imekua na muendelezo mbovu katika Ligi Kuu Bara msimu huu kama ambavyo imekua ikifanya vibaya katika misimu iliyopita.

Kwa miaka ya hivi karibuni Azam imeshindwa kabisa kuonyesha upinzani mbele ya wababe Simba na Yanga licha ya wakati mwingine wakongwe hawa wakiwa katika nyakati mbaya.

Azam Fc imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara moja pekee tangu timu hii ipande daraja mwaka 2008, lakini pia imebeba kombe la FA mara moja tu.


Licha ya uwekezaji mkubwa walioufanya, sajili za wachezaji wakubwa lakini wameshindwa kabisa kujipenyeza katikati ya Simba na Yanga walau kupata nafasi ya pili kama si ubingwa kabisa.

Katika msimu huu pekee mpaka sasa wameshapoteza michezo takribani 8 kati ya michezo 23 waliyoshuka dimbani. Mpaka sasa wanashika nafasi ya tatu wakiwa na alama 32.

Sikiliza uchambuzi yakinifu kutoka kwa Mpwa Tigana Lukinja nini kifanyike Azam Fc iweze kufika kilele cha mafanikio.


Sambaza....