Sambaza....

Rais wa klabu ya soka ya Barcelona Josep Maria Bartomeu amesema mlango upo wazi kwa kocha Pep Guardiola  kurejea tena kwenye klabu hiyo kama atakuwa tayari kufanya hivyo.

Bartomeu amesema alimpa nafasi kocha Guardiola kuendela kuifundisha klabu hiyo baada ya miaka minne ya mafanikio makubwa lakini aliamua kuondoka Camp Nou na kujiunga na Bayern Munich kabla ya kuelekea Manchester City ambapo ndipo anapofundisha hadi hivi sasa.

“Guardiola ana kipaji maalumu, na milango hapa Barcelona ipo wazi kwa ajili yake siku yoyote atakayojisikia kurudi, jana nilisoma sehemu kwamba anataka kurudi hapa katika siku zijazo, kwangu naona ni kitu kizuri, kwani ndio kitu ambapo tulimuomba kabla hajaamua kuondoka kwa sababu ya kuchoka na msukumo uliokuwepo, kurudi kwake itakuwa habari nzuri kwetu,” Bartomeu aliliambia jarida la The Times.

Kati ya mwaka 2008 hadi mwaka 2012 Guardiola akihudumu kama kocha wa Barcelona aliweza kushinda mataji matatu ya ligi kuu nchini Uhispani (La Liga), mataji mawili wa kombe la Mfalme (Copa del Rey) na mataji mawili ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Sambaza....