
Nahodha wa kikosi cha timu ya Taifa ya Burundi, Bigirimana, amewahakikishia kwa uhakika zaidi mashabiki wa nchi hiyo kuwa mechi ya Leo dhidi y Tanzania watashinda. Akiongea na vyombo vya habari jana wakati wa mazoezi ya mwisho ya timu hiyo, amedai wao wamejiandaa kucheza mpira na kuachana na maneo maneno.
”Fyeka Burundi?!… haya ni maneno tu. Tusubirie kazi ya kesho (leo) ndani ya uwanja” Gael Bigirimana aliwaambia waandishi wa habari huku akiilaumu kauli hiyo.
Hii ni kauli mbiu inayotumika na wadau wa mpira nchini katika kuhamasisha ushindi kwa timu ya Taifa, ‘Fyeka Burundi’ mahususi kwaajili ya Burundi kwa sasa.
Kwa upande wa Taifa Stars, wao wapo tayari nnje na ndani ya uwanja pia. Tayari kabisa kwa mchezo wa leo.
Unaweza soma hizi pia..
Mechi Iliyoamua mshindi hatua ya Makundi Kombe la Dunia
Hii ilikuwa ni Kombe la Dunia mwaka 1950, mechi ya Uruguay dhidi ya Brazil. Mechi ambayo iliamua mshindi hatua ya makundi.
Brazil na maajabu ya herufi “R”
Ukiangalia mafanikio ya Brazil kwenye kikosi chao cha mwaka 2002 kulikuwa na wachezaji 8 ambao majina yao yanaanza na R hivyo huwa tunaita kizazi cha "R".
Tanzania kufuzu Afcon ni kama filamu kwetu!
Niacheni nionekane muoga tu lakini akili yangu inampitisha moja kwa moja Algeria kuchukua nafasi moja wapo kati ya hizo mbili.
Taifa Stars yenye nuru
Kocha mkuu wa Taifa Stars ametaja kikosi chake cha Tanzania na huu ni mtazamo wa Tigana Lukinja.