Sambaza....

Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Ahamd Ahmad amesema ameridhishwa na maandalizi ya michuano ya Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON).

Mashindano ya mpira wa miguu kwa Vijana wenye umri wa chini ya  miaka 17 AFCON yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2019 nchini Tanzania.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim jana katika makazi yake, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Wapili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Michezo, Mh Mwakyembe (Kulia), Kutoka kushoto ni Rais wa TFF, Wallace Karia na Rais wa CAF, Ahmad Ahmad.

Pia ameihakikishia Serikali kwamba hakutakuwa mabadiliko yoyote ya ratiba yatakayofanyika kuhusu wenyeji wa mashindano na kwamba CAF itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kufanikisha michuano hiyo.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mechi zote za michuano ya Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON) zitafanyika jijini Dar es Salaam.

“Tupo katika hatua za mwisho za maandalijzi ya michuano hiyo itakayofanyika jijini Dar Es Salaam katika viwanja vya Taifa, Uhuru, Chamanzi na JK Park utatumika kwa mazoezi.” Majaliwa amesema.

Waziri Mkuu amesema ni muhimu kwa nchi kushiriki katika mashindano makubwa kama hayo kwa kuwa yanasaidia kwenye ukuzaji wa vipaji kwa vijana ambao wengi wao ni wanafunzi.

Sambaza....