Bakari Nondo, Ibrahim Ame, Soud Dondola
Ligi Kuu

Coastal Union na rekodi isiyoimbwa!

Sambaza....

Coastal Union “Wagosi wa Kaya” kutoka Tanga mpaka Ligi ikiwa inasimama kutokana na ugonjwa wa Corona inashika nafasi ya 5 ikiwa na alama 46 huku ikiwa chini ya Simba, Azam, Yanga na Naungo fc iliyowaacha kwa alama 4 tu.

Katika msimu uliopita Coastal kwa nyakati kama hizi haikua katika nafasi nzuri huku wakiwa ni miongoni mwa timu zilizo katika hatari ya kushuka daraja. Lakini msimu huu imeonekana kuimarika na kutotaka kabisa masihara katika Ligi huku ikitoa kipigo mara kwa mara katika uwanja wake wa Mkwakwani.

Walinzi wa kati wa Coastal Union Ibrahim Ame na Bakari Mwamunyeto.

 

Uimara wa Coastal unatokana na eneo la ulinzi ambapo kwa kiasi kikubwa wameweza kucheza vyema na kuwathibiti washambuliaji wa timu pinzani. Eneo la ulinzi wa Coastal lipo chini ya nahodha Bakari Mwamunyeto na Ibrahim Ame ambao kwa kiasi kikubwa wametekeleza.

Soud Dondola mlinda mlango wa Coastal amekua  akilindwa vyema na safu ya walinzi kina Mwamunyeto, Ame, Hance Masoud na Aboubakar Kinanda na kiungo wa ukabaji Mtenje Albano.

Mtenje Albano akimthibiti mshambuliaji wa Polisi Tanzania fc.

Mpaka sasa Coastal Union imefungwa mabao 20 huku wao wakiwa wamefunga mabao 28 lakini cha kuvutia zaidi ni uwezo wa kipa Soud Dondola kupata “clean sheet” nyingi mpaka sasa. Mlinda mlango huyo Soud Abdalah Dondola amefanikiwa kucheza michezo 13 bila nyavu zake kutikiswa na hivyo kua na mchango mkubwa katika kuifikisha Coastal katika tano bora ya VPL.

Rekodi hiyo ya Soud Dondola kwa hakika inasaidiwa na kiasi kikubwa na mbinu za mwalim wa timu ya Taifa na mchezaji wa zamani wa Coastal Union Juma Mgunda  na kocha msaidizi Lazaro.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.