David Molinga "Falcao"
Blog

David Molinga ampigia goti Mkwasa

Sambaza....

Baada ya kutolea halo ya kutoelewana kati ya kocha msaidizi wa Yanga na mshambuliaji wa Yanga,  David Molinga , jana jioni David Molinga mbele ya wachezaji wa Yanga , viongozi wa Yanga na GSM aliomba msamaha.

David Molinga aliwaomba radhi wachezaji wenzake pamoja na kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa kwa utovu wa nidhamu. Uongozi wa Yanga SC na wadhamini wao GSM walihudhuria kikao hicho cha kuombana msamaha .

David Molinga akipambana na Abdalah Mfuko wa KMC

Charles Boniface Mkwasa na David Molinga walipishana baada ya Charles Boniface Mkwasa kumwondoa kwenye kikosi cha Yanga kutokana na David Molinga kukosa “fitness” kwa sababu ya kuongezeka uzito.

Kitendo cha kuondolewa kwenye kikosi hicho kilimkwaza David Molinga mpaka kufikia hatua ya yeye kuongea na vyombo vya habari na kudai kuwa Charles Boniface Mkwasa hampendi David Molinga.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.