Ligi Kuu

DITRAM NCHIMBI alikuwa beki wa kwanza wa YANGA

Sambaza....

 

Jana katika mchezo dhidi ya Simba kocha wa Yanga Charles Boniface Mkwasa aliamua kuanza na mshambuliaji mmoja wa kati huku nyuma yake akiwa anacheza Papy Kabamba Tshishimbi.

Charles Boniface Mkwasa alianza na mfumo wa 4-4-1-1 ambapo alijaza viungo wengi wenye asili ya katikati , Makame , Mapinduzi Balama , Mohamed Banka, Haruna Niyonzima na Papy Kabamba Tshishimbi huku Ditram Nchimbi akiwa kama mshambuliaji peke yake.

 

Upi ulikuwa umuhimu wa Ditram Nchimbi hasa hasa kipindi cha kwanza ? Boniface Mkwasa alijua Simba hupenda kuanzisha mashambulizi yao nyuma , mabeki wa kati ndiyo huwa wanaanzisha mashambulizi.

Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli la pili lililofungwa na Mo Banka

Ditram Nchimbi alikuwepo pale kupambana nao ili wasiwe huru kuanzisha mashambulizi kutokea nyuma , kitu ambacho kiliwafanya mabeki wa kati wa Simba wasifanikiwe kupiga pasi nyingi sana kama ilivyozoeleka.

Kuna wakati alikuwa anashuka mpaka katikati kupambana na viungo wa Kati wa Simba , alikuwa kiunganishi kikubwa kwenye eneo la ukabaji wa juu katika kikosi cha Yanga cha jana yeye ndiye alikuwa beki wa kwanza.

Sambaza....