Amunike
Blog

Emmanuel Amunike aula tena !

Sambaza....

Alitupa furaha ambayo tulikuwa tunaisubiri kwa muda mrefu , miaka 39 ndiyo miaka ambayo ilitufanya tusubiri ili twende kwenye michuano ya mataifa huru ya Africa (Afcon).

Mwaka 2019 ndiyo mwaka ambao tulipata furaha kubwa , furaha iliyochagizwa na Emmanuel Amunike , huyu ndiye aliyekuwa kiongozi imara kutuongoza mpaka Afcon tuliyokaa miaka 39 bila kwenda.

Baada ya michuano hii ambayo hatukufanikiwa kupata hata alama moja kwenye michuano hii tuliamua kuachana na kocha huyu ambaye alikuwa kocha mkuu wa timu yetu ya Taifa “taifa stars” Emmanuel Amunike .

Rasmi kwa sasa kocha huyu atakuwa kocha mkuu wa timu inayocheza ligi kuu ya Misri inayoitwa El-Makkasa na atakuwa analipwa kwa pound ya Misri ya 15K.

El-Makkasa inashika nafasi ya kumi na tano (15) kwenye ligi ambayo ina timu kumi na nane (18) , kazi kubwa aliyonayo Emmanuel Amunike ni kuhakikisha El-Makkasa inabaki kwenye ligi kuu ili ikishuka daraja.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.