Stori

Gift Mauya! Zawadi ya kweli katika ulimwengu wa soka!

Sambaza....

Mwanangu kuwa uyaone, si maghorofa ya kariakoo wala mawe ya mwanza, bali na zawadi mbalimbali zilizopo ulimwenguni.
Ulimwengu wa soka ‘Tanzania’ unaimani kubwa kwa uwezo wa viungo wa timu zao pendwa Simba na Yanga kuliko wachezaji wa timu nyingine.

Kumbe sio kweli unapotoka, haujui kuwa kule Kagera Sugar kuna zawadi moja iliyoshushwa kuja kuwafurahisha na kuwafaidisha wanasoka, na wazazi wa kijana huyo walilijua hilo toka anazaliwa ndio maana wakampatia jina la Zawadi.

Zawadi Peter Mauya, kiungo wa mpira dimba la chini, anatema kulia anafukia kushoto, anakata umeme wa tanesco anawasha “Generator” imara mithili ya zile za hospitali kubwa kubwa.

Zawadi Mauya na Abdallah Sesseme

Ni miaka mingi imepita sijaona kiungo wa dimba la chini ‘Defensive midfilder’ nguvu kadhaa akili nyingi, wengi wao ni nguvu kwanza akili baadae, Zawadi hayupo hivo, kama kuna mwingine umjuae nitajie.

Mipango yote ya ile ‘sex football’ wanayotandaza Wanankurukumbi wale inaanzia kwake akipata mpira anaficha kwanza kisha anawastua Seseme, Awesu na Ally Kagawa anawambia ‘wazee mali hii hapa, chukueni muifanye mnavyotaka’ kinachofuata hapo ni kampa kampa tena na vidude kibao, binafsi jamaa namfananisha kama Andre Pirlo yulee wa Juventus ya Turin.

Zawadi Mauya katikati akiwa na MwaitaGereza, Hassan Isihaka (kulia) pamoja na Peter Mwalianzi, Abdallah Sesseme (kushoto).

Waumini wa falsafa ya ‘Mpira kucheza’ wananambia Zawadi asiondoke pale Kagera, abaki azidi kuwatesa timu pinzani na kuwapa burudani wana kagera.

Lakini Waamini wa ‘Mpira Pesa/maendeleo’ wao wananiamba Gift atoke Kagera aingie timu kubwa zaidi Simba, Yanga, ama Azam avune matunda ya miguu yake kwa ukubwa zaidi na iwe tiketi ya kukipiga nje ya nchi hii, yaani Kimataifa.

Mimi sio wakala wala dalali, hivyo nimetulia zangu nakula upepo na kumtizama fundi huyu wa kandanda ataamua nini.

Sambaza....