EPL

Goli la Son laweka rekodi mpya Spurs.

Sambaza kwa marafiki....

Mkorea Huen Min Son amefanikiwa kuandika historia mpya kwa klabu yake ya Totenham Hotspurs baada ya ushindi wa bao mbili bila mbele ya majirani zao wa London Crystal Palace katika EPL.

Son anakua mchezaji wa kwanza kufunga goli katika uwanja mpya wa nyumbani wa Spurs unaojulikana kwa jina la Totenham Hotspurs Stadium. Son amefunga goli hilo dhidi ya wapinzani wao wa jiji moja wanaotokea London Kusini  Crystal Palace .

Son alifunga goli hilo katika dakika ya 55 baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Christian Eriksen. Lakini pia Eriksen licha ya kutoa msaada na yeye alifanikiwa kufunga bao la pili kwa Spurs. Mpaka mchezo unamalizika Totenham wamepata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri hivyo kuufungua uwanja kwa ushindi mnono.

Tafadhali tumia viungo rasmi kusambaza habari zetu. Facebook, Twitter au Barua Pepe. Kama utataka kutumia habari zetu tuandikie kupitia habari@kandanda.co.tz