Shirikisho Afrika

Hamkutaka tumkokee moto babu yetu Onyango!?

Sambaza....

Speaking about Uchawi kwenye Mpira ni saikolojia ambayo mkicheza na watu wanaoamini kwenye Uchawi lazima itawatesa akili yao!

Pirates ni moja ya Timu inayoamini sana kwenye “Shirki” aka “Juju” wenyewe Wazulu wanaita “Muthi” . Walipokuja pale Lupaso kijijini kwa Benja walifanya kila kitu kinachoashiria Shirki!

Walimwaga maji kwenye kila walipokanyaga, walimwaga maji kwenye uwanja walipoingia kwenye magoli yote mawili na katikati ya uwanja. Ukikutana na mpinzani wa namna hii rahisi sana kumu-win kwenye upande huo wa Saikolojia!


Walikuja na maji kwenye nchi ya joto tukaenda na moto kwenye nhi ya baridi ila nashangaa vilio vimekuwa vingi saana kwahiyo hamkutaka Tumkokee Moto Babu yetu Onyango?

NB: CAF wanatakiwa watoe adhabu kwenye haya Mambo kama inavyofanya TFF.

Sambaza....