Zahera
Blog

Hatumfukuzi Zahera , Mashabiki tulieni!

Sambaza kwa marafiki....

Baada ya maneno mengi kutoka kwenye mitandao ya kijamii kuhusu hatma ya kocha mkuu wa Yanga , Mwinyi Zahera ambaye yuko kwenye shinikizo kubwa kutoka kwa mashabiki ambao wengi wanataka aondoke baada ya kufanya vibaya dhidi ya Pyramid FC.

Afisa Habari wa Yanga , Hassan Bumbuli amedai kuwa nayo ni maneno ya kwenye mitandao tu na uongozi mpaka sasa hivi haujaamua kuhusu hatma yake. “Kwa sasa acha yabaki maneno ya mitandaoni lakini uongozi wa Yanga haujakaa kufikia hatua ya kumfukuza kocha mkuu Mwinyi Zahera”.

“Mashabiki wangetulia kwa sasa kwa sababu kocha wao mkuu mpaka sasa hivi ni Mwinyi Zahera hivo wangeruhusu utulivu”. Alimalizia kusema Afisa Habari huyo wa Yanga ambaye amedai mpaka sasa hivi hawajatoa taarifa ya Mwinyi Zahera kufungwa. Yanga ilifungwa na Pyramid FC ya Misri , matokeo ambayo yamekuja na shinikizo la kumfukuza Mwinyi zahera

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.