Blog

Jezi tata Old Trafford

Sambaza....

Magwiji kadhaa wamepita, wakaitumia na kuifanyia mambo makubwa na kuifanya iwe jezi yenye heshima pale Old Trafford, baadhi ya magwiji hao ni pamoja na Eric Cantona, David Beckham na Cristiano wa Juventus

Lakini tangu Cristiano aondoke jezi hii haijampata mrithi sahihi wa kuivaa mpaka muda huu, wapo waliojaribu na wameishia kufeli, swali linaloniumiza kichwa ni je kwa miaka hii ya karibuni hakuna mchezaji mzuri wa kwenda kuitendea haki au laa? Nakosa majibu

Nikijaribu kuvuta kumbukumbu nakumbuka mwaka 2014 United ilimsajili Angel di Maria aliyekuwa na kiwango bora akitokea Real Madrid kwa ada ya £59.7 M, wengi tukajua Jezi imepata mvaaji, lakini msimu ule majeraha yalimpenda na kiwango chake hakikuwaridhisha sana mabosi wa United, na wakamuonesha mlango wa kutokea kwenye viunga vya OT na kumpeleka PSG kwa dau la £44.3 M. Najiuliza je united walifanya kitu sahihi, kwa nini wasingempa muda kuona msimu wake wa pili ungekuwaje, sipate majibu

Katika pitapita zangu kwenye mitandao ya kijamii nikakutana na kijana Memphis Depay akiwa katinga jezi yake ya Man U no 7 mgongoni. Nikakumbuka alisajiliwa kutoka PSV kwa ada ya £25 M akionekana kuwa mrithi wa CR7. Na yeye kama ilivyokuwa kwa di Maria, kiwango chake hakikumridhisha Jose Mourinho aliyeamua kumpiga panga kwenye kikosi chake. Akaenda kujiunga na Lyon ambako huko anawasha moto mpaka sasa. Hapa jibu nililolipata ni kwamba Mou hapendi ubishoo

Sanchez akiwa na jezi namba 7

Alexis Sanchez kwenye kiwango bora kabisa akiwa Arsenal huku mkataba wake ukielekea ukingoni akaweza kuyavutia macho ya mahasimu wawili Pep na Jose, lakini sijui ni tamaa ya pesa ikamfanya anase kwenye chambo ya Mou akifanyiwa swap na Mikhitaryan. Kiwango chake hakijawa kizuri tangu ajiunge na United, mwanzoni nilijua ni mfumo au ana bifu na Mou, lakini nikikumbuka Mou ana miezi kadhaa hayupo OT napata ukakasi wa nini tatizo la Sanchez

Kocha wa zamani wa Man Utd, Sir Alex Ferguson (Kushoto) akiwa na David Beckham

Nawaza au Sir Fergie ana jicho ambalo makocha wengine hawana? Au ni muda sasa wa kuistaafisha ile jezi ili isiendelee kuwapa presha wachezaji wengi pale OT?

Mawazo yangu yananipeleka mbali ambapo kurudi nimeshindwa hata sielewi ni nini tatizo


-imeandaliwa na Seif Mahmoud

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x