Ligi Kuu

Kandanda yaendelea kumwaga tuzo, ni zamu ya Chirwa

Sambaza....

Tovuti ya Kandanda.co.tz imeendelea na utaratibu wake wa kusheherekea na wachezaji pamoja na timu zinazofanya vizuri katika Ligi Kuu Bara sasa ikiwa zamu ya Galacha wa Hatrick.

Obrey Chirwa

Obrey Chirwa amekabidhiwa zawadi yake ya Galacha Oyee baada ya kuibuka Galacha wa Hatrick katika msimu 2019/2020 uliomalizika. Chirwa alifunga hatrick mbili katika michezo miwili tofauti ya Ligi Kuu. Hatrick ya kwanza alifunga katika uwanja wa Nyamagana dhidi ya Alliance na Hatrick ya pili alifunga dhidi ya Singida Utd katika dimba la Chamanzi.

Nizar Khalfani akimkabidhi Tunzo ya Galacha wa Hatrick mshambuliaji wa Azam fc Obrey Chirwa.

Nyota huyo wa Azam fc alikabidhiwa zawadi yake katika ufunguzi wa wiki ya Azamfc iliyofanyika katika uwanja wa Chamanzi na nyota wa zamani wa Vancoover Whitecaps ya Canada, Yanga na Timu ya Taifa Nizar Khalfani.

Baada ya kupokea tuzo hiyo Chirwa hakusita kuishukuru tovuti ya Kandanda na kusema ni zawadi muhimu katika maisha yake ya soka.

Kutoka kushoto Thomas Mselemu (Afisa masoko wa Kandanda.co.tz), Obrey Chirwa (Galacha wa Hatrick msimu 2019/2020), Nizar Khalfan (Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa), Tigana Lukinja (East Africa Tv&Radio) na Zakaria Zaka za Kazi (Msemaji wa Azam fc)

Chirwa ” Namshukuru Mungu hii tuzo naipokea vizuri, tunzo nzuri nimegombea na wachezaji wengi tofauti tofauti, imebalance kwangu kwenye kabati la tuzo zangu.”

 

Sambaza....