Ligi Kuu

Kandanda yampa nguvu Kagere ya kuwaua makipa!

Sambaza....

Kwa misimu miwili mfululizo mshambuliaji wa Simba , Meddie Kagere amefanikiwa kuwa mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania bara. Ndani ya misimu hiyo miwili amefanikiwa kufunga magoli 45.

Leo hii Mtandao wa kandanda.co.tz umefanikiwa kukabidhi tuzo ya Galacha wa magoli msimu wa 2019/2020 baada ya kuibuka mfungaji bora akiwa na magoli 22. Tuzo hiyo imetolewa na Bi. Margy Simalenga, Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kampuni ya huduma za kusafirisha vifurushi, EMjey Courier company.

Baada ya kupewa tunzo hiyo Meddie Kagere alitoa neno la shukurani.

“Namshukuru Mungu kwa kupata tuzo ya mfungaki bora mara mbili mfululizo. Nawashakuru pia wachezaji wangu kwa kujituma. Mimi kupata hii tuzo haimanishi nimepata peke yangu ila tumesaidizana kujituma na wachezaji wenzangu”.

Meddie Kagere alipoulizwa kuhusu ubora wake alidai kuwa hawezi kusema kuwa yeye ni bora ila kwa sababu mpira ni mchezo wa makosa ndiyo maana anaonekana bora kwa kuyatumia makosa.

“Siwezi kusema mimi ni bora. Ndiyo maana wanasema ni “game of football” wote tuna enjoy , watu wanafanya makosa kusingekuwepo hakuna makosa tusingeona hii ladha ya huu mchezo , hata kama ukiwa bora kiasi gani lazima ufanye makosa.

Ndiyo maana mshambuliaji ninaweza kukosa nafasi ya wazi kabisa. Hivo hivo beki anaweza kufanya makosa na mshambuliaji akayatumia hayo makosa. Kwa hiyo msimu ujao mabeki watajiandaa na mimi kwa sababu washanizoea niko hivi nitajiandaa kitu kipya ili kuleta ladha ya mchezo”. Alisema Meddie Kagere.

Kuhusu tuzo ya Galacha wa magoli kutoka mtandao wa Kandanda.co.tz amesema kuwa tuzo hiyo inampa nafasi ya kupigana zaidi.

“Hii tuzo itanipa nguvu kama mshambuliaji hii ni “motivation” inanipa nafasi ya kupigana mara kwa mara ili kupata tunzo nyingine. Hakuna kusema inatosha hata hela zenyewe ukiwa bilionea utazidi kutafuta hutosema umetosha.

Hii ni kazi yangu kwa hiyo kupata hii tuzo kunanifanya nifunge zaidi na zaidi kwa sababu hii ni kazi yangu na tunzo hii inanipa motisha”- alimalizia Meddie Kagere.

Meddie Kagere kwa misimu miwili mfululizo amekuwa mfungaji bora. Msimu wa mwaka 2018/2019 aliibuka Galacha wa magoli kwa kufunga magoli 23.

Meddie Kagere (Simba Sc

Msimu wa mwaka 2019/2020 aliibuka mfungaji bora na amechukua tunzo ya Galacha wa magoli kutoka mtandao wa kandanda.co.tz. Kagere pia ametwaa jozi mbili za viatu katika kusheherekea kwa kufunga magoli mengi katika miezi miwili tofauti, tuzo ambayo mtandao wetu ulishirikiana na Mgahawa Cafe & Restaurant.

Kipekee mtandao wa Kandanda unatoa shukurani kwa mdhamini mkuu wa Galacha wa Magoli, Mgahawa Cafe & Restaurant, pamoja na SeeBait, 98 Minutes kwa ushirikiano wao na kutuwezesha. Pia inatoa shukurani kwa viongozi na wachezaji wa timu mbalimbali za ligi kuu kwa kutoa ushirikiano msimu uliopita.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.