Sambaza....

Bado hujacheza Kariakoo, jezi uliyopewa ni nzito na mtu wa mwisho kuivaa alikuwa bora hasa, timu inahitaji mafanikio na presha ni kubwa kwa wakati huo. Nani anakuamini kukupa nafasi moja kwa moja?

Hii ilikuwa karata ngumu sana kwa Wananchii kuicheza ndani ya klabu yao kwa wakati ule! Ni wakati ule ambao hawana Kelvin Yondani wala Nadir Haroub “Canavaro” katika eneo lao la ulinzi lakini bado waliamini kuna kitu kipya kutoka pale Morogoro.

 

Mezani kuna Jina la Dickson Job kutoka Mtibwa Sugar pale Morogoro! Young Africans chini ya Eng. Hersi Said wakaona isiwe shida wakatoa pesa na kwenda kuchukua mchezaji lengo ni kuleta sura na damu mpya kwenye eneo la ulinzi.

Hapa kuna kipaji, imani na muda ambao Young Africans waliamini vyote vinapaswa kuishi ndani ya “Big Brain Defender”!. Narudia tena ilikuwa karata ngumu sana lakini imewalipa kwa kiasi kikubwa mpaka hivi sasa pale Jangwani hakuna presha tena.

Dickson Job kipaji kipo na ameonyesha hilo, imani kutoka kwa viongozi wa Young Africans kwenda kwake ilikuwa kubwa na amewalipa fadhila huku muda aliopata ndani ya uwanja umeipa timu mafanikio! Yes it’s simple to call his “Big Brain Defender”.

Dickson Job akimthibiti mshambuliaji wa USM Algier katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika

Binafsi kwa sasa namuelewa sana Miguel Gamondi anavyojaribu kufanya “Rotation” kati ya Job na Nondo kwenye eneo la ulinzi huku Ibrahim Bacca akitumika sana kuliko hawa wawili. Why? Nadhani wametumika sana miaka miwili iliyopita wanahitaji kupumzika kwa baadhi ya mechi pia msimu huu.

Dickson Job kuna muda alitumika kama beki wa pembeni na alicheza kwa usahihi achilia mbali baadhi ya mechi chache ambazo amewahi kucheza kama namba 6! Hakuna timu ambayo haitamani kuwa na mchezaji wa aina hii kwenye eneo la ulinzi kila timu inatamani sana.

Kiwango chake kipo kwenye mwendo mzuri tangu yupo chini ya Mohamed Nabi mpaka sasa kwa Miguel Gamondi! Akianzia benchi au asipocheza akacheza mechi inayofuata bado atakupa dakika nzuri sana uwanjani, namuelewa sana kocha kumpumzisha baadhi ya mechi sababu msimu uliopita katumika sana uwanjani.

Good Signing for Young Africans within this three years! Umri mdogo na kipaji kikubwa hii ni pesa kwa Wananchii na hadhina kubwa kwa Taifa la Tanzania.

Sambaza....