Wachezaji wa Serengeti Boys wakipata maelezo kwenye moja ya mechi
Blog

Kelvin John kucheza Ulaya

Sambaza kwa marafiki....

Nyota ya Kelvin John itawaka zaidi muda si mrefu. Katika mahojiano aliyofsnya na kandanda, Kelvin alituambia watu wanaosimamia kazi zake wanaendelea kupambana mara tu baada ya michuano ya AFCON.

Kwa utulivu kabisa Kelvin alisema “Kuna vitu ambavyo watu ambao wananisimamia mimi wapo kwenye mazungumzo na timu nyingi, mpaka sasa hivi mimi kama mchezaji niko tayari kucheza timu yoyote ambayo Etoo amenichagulia.” Ikumbukwe kuwa Kelvin anamawasiliano ya karibu na Ssmuel Eto’o, mchezaji wa zamani FC Barcelona.

Kumekuwa na mawasiliano ya mata kwa mars kati yake na Samuel Eto’o, kwakuwa pia alimuangalia wakati wa michuano ya AFCON. Na kama Serengeti Boys ingefika mbali basi tungepata matunda zaidi.

Kwa maendeleo ya kipaji chake na soka letu kwa sasa tunasubiri kujua Kelvin John ataelekea wapi, wakati mameneja wake wakiendelea lushughulikia swala lake kupitia Samuel Eto’o.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.