Zamani tulikuwa na kundi dogo la wachezaji wanaocheza nje. Hawakuwa wanafika hata watano, lakini hivi sasa tunaweza kuita wachezaji 17 wanaocheza nje bila kujumuisha wachezaji wa ndani.
Kwa maendeleo ya kipaji chake na soka letu kwa sasa tunasubiri kujua Kelvin John ataelekea wapi, wakati mameneja wake wakiendelea lushughulikia swala lake kupitia Samuel Eto’o.
Fuatilia sehemu ya kwanza ya mahojiano na Kelvin John, mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 (Serengeti Boys).