Kevin Kongwe Sabato "Kevi Kiduku".
Ligi Kuu

Kevin Sabato: Marcel Boniventure ni zaidi ya Chama

Sambaza....

Mshambuliaji mwenye kasi, nguvu na msumbufu kwa mabeki Kevin Kongwe Sabato ambae kwasasa anaitumikia Kagera Sugar amemataja Marcel kama hazina kubwa kwa Taifa kutokana na uwezo mkubwa alionao.

Kandanda ilipata wakati wa kupiga story mbili tatu na Kevi Kiduku na kumtaja Kaheza kama mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu ambae kama mshambuliaji ukicheza nae ni lazima utafunga tuu magoli.

Marcel Kaheza Boniventure akiwa katika uzi Majimaji fc.

Kevin Sabato “Nakumbuka goli langu ambalo sitolisahau katika soka mpaka sasa wakati  nipo Majimaji nililowafunga Mbeya City katika uwanja wa Majimaji Songea, pasi alinipigia Kaheza.

Yule jamaa anajua sana mpira na ni mzuru katika kutengeneza nafasi za kufunga. Marcel anajua sana mpira hata yule Chama wa Simba hajamzidi kitu basi tuu kipindi kile anakwenda Simba (Marcel Kaheza) mambo hayakumwendea sawa kutokana na vitu flani. Lakini ni moja ya wachezaji wazuri kuwahi kucheza nae.”

Marcel Boniventure Kaheza

Kevin Sabato na Marcel Kaheza walicheza wote katika klabu ya Majimaji ambapo Kevi alijiunga na Majimaji katika dirisha dogo akitokea Mwadui fc. Ambapo Kevi alifanikiwa kuinusuru Majimaji isishuke daraja katika msimu wa 2016/2017.

Marcel Boniventure Kaheza “Rivaldo” kwasasa anakitumikia kikosi cha  Polisi Tanzania akijiunga nao akitokea Simba sc iliyomtoa kwa mkopo.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.