Shafiq Batambuze
Ligi Kuu

Kikosi bora chá VPL cha wachezaji waliosahaulika!

Sambaza....

Ligi Kuu Bara imeshapata bingwa tayari huku tukisubiri watakaoshuka daraja na kuwapisha waliopanda daraja KMC, JKT Tanzania, Coastal Union, African Lyon, Biashaara na Allience School.

Baadhi ya wachezaji waliopo katika timu zilizopo katika nafasi za juu (Simba, Yanga na Azam ) wamepigiwa  chapuo kua katika kikosi bora na kugombea tuzo mbalimbali  msimu huu.

Tovuti yako ya kandanda.co.tz inakuletea nyota bora 11 waliotoa mchango mkubwa katika timu hata kama hawajapata ubingwa wala hawapo katika nafasi za juu.

1. Aron Kalambo- Tanzania Prisons!

Mchezaji wa zamani wa CDA ya Dodoma amekua moto wa kuotea mbali msimu huu katika kikosi cha Prisons, huku akiwa kipa aliecheza mechi nyingi nyuma ya Aishi Manula wa Simba.

2. Salum Kimenya – Tanzania Prisons!

Amekua mchezaji muhimu katika kikosi cha “wajelajela” katika beki wa kulia kabla ya kocha Barresi kumbadili nafasi na kumpeleka eneo la ushambuliaji au kiungo wa kulia.

3. Shafiq Batambuze – Singida united!

Beki wa kushoto aliekamilika unaweza kusema katika VPL. Kitu pekee kilichomuangusha mbele ya Asante Kwasi  ni mafanikio ya Simba pia uwezo wa kufunga wa Kwasi.

4. Ally Ally -Stand United!

Beki imara alieiongoza Stand katika mapambano ya kushuka daraja na kuweza kuinasua katika nafasi za chini na kuiweka salama. Simba wanamkumbuka vizuri  katika mechi ya raundi ya pili uwanja wa taifa.

5. Kennedy Juma – Singida utd!

Licha ya ugeni wa ligi lakini aliweza kuweka ukuta imara kwa walima alizeti hao na kupeleka kumshawishi kocha kumjumuisha katika kikosi cha timu ya (Kilimanjaro) kilichoshiriki michuano ya Challenge nchini Kenya.

6. Ally Nasoro Ufudu – Kagera Sugar!

Mwanzoni mwa msimu Kagera Sugar ilianza vibaya lakini wakaja kukaa sawa na kukwepa kushuka daraja. Ufudu ameweza kusimama imara katika eneo la kiungo na kuweza kuisaidia Kagera kusalia Ligi Kuu Bara.

7. Hamis Mcha – Ruvu Shooting!

Tangu ajiunge na maafande hao amekua na msaada katika kikosi hicho cha Masau Bwire na kuibuka mchezaji muhimu katika mtindo wao wa “Kupapasa” huku yeye akiwa mfungaji bora katika kikosi hicho.

8. Hassan Dilunga – Mtibwa Sugar!

Ni kama amezaliwa upya baada ya kupotea tangu atoke  Yanga, akiwa na Mtibwa amekua na kiwango imara huku akifunga magoli muhimu ya Mtibwa Sugar msimu huu.

9. Eliuta Mpepo – Tanzania Prisons!

Ni kama amekua mrithi sahihi wa Jeremiah Juma na kuweza kufunga magoli 10 mpaka sasa huku akiwa bado mchezaji chipukizi. Kwa kiasi kikubwa ameweza kuisaidia Prisons kumaliza katika nafasi za juu.

10. Marcel Boniventure – Majimaji FC!

Ni kama mwanajeshi aliejivika mabomu katika msitu wa vita. Bado anaipigania Majimaji isishuke daraja huku akiwa mzawa pekee aliefunga magoli matatu katika mechi moja, katika mchezo wa Majimaji dhidi ya Ruvu Shooting.

11. Mohamed Issa – Mtibwa Sugar!

Moja ya viungo maridadi na waburudishaji katika VPL. Amekua na kiwango kizuri mpaka kupeleka kujumuishwa mara kwa mara katika timu ya Taifa msimu huu.

Sub:

1. Jnr Manyika (Singida utd), 2. E. Mlilo (Stand Utd) , 3. A. Mfuko (Mwadui), 4. M. Nampaka (Lipuli fc),  5. Babu Ally (Mbeya City), 6. A. Salamba (Lipuli fc)  7. H. Kyombo (Mbao fc.)

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x