Mataifa Afrika

Kim na matumaini mapya kwa Watanzania

Sambaza....

Sare ya ugenini ya bao 1-1 ya Taifa stars dhidi ya wenyeji Niger imeleta mtizamo wenye matumaini makubwa kufuzu michuano ya AFCON kwa mwaka 2023 nchini Ivory Coast.

Ni kama tumeanza vizuri kama ambavyo tulianza vizuri kwa sare ya ugenini dhidi ya majirani zetu Uganda katika kampeni ya mwaka 2019 kwenda nchini Misri na tukaihitimisha kwa kufanikiwa kushiriki.

Nyoni akitetema baada ya kufunga penati katika mchezo dhidi ya Uganda iliyopelekea Tanzania kufuzu Afcon nchini Misri.

Benchi la ufundi la timu ya Taifa inayoongozwa na Mdenishi Kim Poulsen akisaidiwa na nyota wazamani wa timu hiyo Shadrack Nsajigwa na Ivo Mapunda pamoja na Nadir Haroub “Canavaro” akiwa ni meneja wa timu.

Walijipanga vizuri kiufundi kimbinu na kisaikolojia kuweza kupata angalau alama moja kama itashindikana zote tatu.

Kim Polsen.

Uteuzi wa wachezaji walioanza ulikuwa mzuri sana kwa akili na maarifa ya mbinu za ulinzi zaidi (defensive mentality)kama Himid Mao.

Pia kuwa na viungo wengi wenye majukumu tofauti ya ufanyaji kazi kwa mfano Novatus Dismas kucheza kwa aina ya kiungo mkabaji na kutengeneza “piston” mbili zenye ubora kwenye ulinzi wa kati huku wakisaidiwa na piston mbili za juu ambapo ni Feisal Salum na kiungo wa pembeni mualikwa Simon Msuva ambapo walikuwa na nidhamu kubwa sana kwenye matukio yote matatu ya uwanjani “defensive, offensive na transition.”

Novatus Dismas (kushoto) na Feisal Salum (kulia).

Kwenye eneo la “Transition speed” ilikuwa ya hali ya juu hasa umri ya wahusikia na asili yao ya kiuchezaji kama vile Msuva, Fei wamekuwa sifa ya kasi siku zote.

Washambuliaji wawili walioorodheshwa kwenye kikosi Mbwana Samatta na George Mpole walianza kutimiza majukumu yao mapema kabisa kwenye dakika ya kwanza kwa goli zuri hali iliyomfanya muda mwingine moja kutoka na kwenda kwenye eneo la kati kusaidia timu na kufanya mfumo kuonekana kama ni 5-4-1.

Wachezaji wa Stars wakishangilia goli katika mchezo dhidi ya Niger lililofungwa na George Mpole.

Lakini walikumbuka kuungana na yule moja aliyekuwa anabaki mbele mara wakipora mpira na kufanya “transition” ya haraka.

Mashambulizi ya muunganiko na ya kushtukiza  yaliwafanya Niger kuwa na nidhamu ya ulinzi na kuwalazimisha mabeki wao kitokupanda kuongeza nguvu kwa washambuliaji wao.

Kim alifanikiwa pia kuwabana kwenye idara ya kiungo kwa idadi ya wachezaji na kuwalazimisha wenyeji kubadili mpango wao wa mechi  wapite pembeni na siyo kati mwa uwanja.  Hata goli lao lilitokana na krosi ya kutoka kaskazini magharibi ya uwanja na siyo katikati.

Wachezaji Stars walioanza kikosi cha kwanza wakipasha mwili kabla ya mchezo.

Dhana ya ubora katika uteuzi wa kikosi na mpango kazi wa kufanya ilikuja kutimizwa vyema na mchezaji mwenye nguvu na kasi Kibu Denis aliyehifadhiwa kwa ajili ya mbinu ya pili (Plan B) alivyoingia alikuta energy ya timu inapungua hivyo yeye mwenye nguvu mpya akaboost kitu ambacho kilikwenda kufanyika vyema kabisa

Tunamuona kwenye kupiga kross maridhawa ambayo haikumaliziwa na mtu na ile iliyogonga nguzo yote yangeweza kuwa magoli kama kungekuwa na mwezake kwa wakati sahihi

Wakati Stars inawashambulia ilifanya timu ya Niger ikatika na kuwa faida sana kwetu licha wa wao kushambulia mara chache chache.

Sambaza....