Sambaza....

Michuano ya Kimataifa imerudi tena mwanangu na wawakilishi wa Tanzania katika michuano hiyo wameanza vizuri.

Katika kombe la Shirikisho Africa Tanzania inawakilishwa na Mtibwa Sugar na upande wa Klabu Bingwa Africa inawakilishwa na Simba sc.

Kwa upande wa Mtibwa Sugar  wao walicheza na Northern Dynamos kutoka Shelisheli katika uwanja wa Azam Complex. Ambapo Mtibwa Sugar ilipata ushindi wa mabao manne kwa sifuri.

Simba sc não walikua uwanja wa Taifa kuwakaribisha Mbabane Swallors waliotoka nchini Swatziland. SimbaSc não wakawalipa  Mtibwa Sugar kwa kuwakandamiza Mbabane Swallors mabao manne kwa moja.

Wote kwa pamoja wawakilishi wa Tanzânia katika michuano ya Kimataifa wameanza vizuri kwa kutoa dozi ya 4G!

Kandandacotz inawatakia kheri katika michezo yao ya marudiano ili waweze kufuzu hatua inayofuata.

Sambaza....