Ligi Kuu

Kipa Dodoma katolewa tuu kafara!

Sambaza....

Nimetizama game ya Jana ya Dodoma jiji dhidi ya Wananchi ambayo wageni walipata ushindi wa bao 2-0. Gumzo kubwa ni aina ya magoli yaliyofungwa katika mchezo huo yote yakiwa ya mbali au unaweza kusema nje ya 18.

Kitu kinachoonesha Yanga walifanyia kazi mkwamo wao wa kutikisa nyavu katija mechi tatu mfululizo na matokeo  yake inawezekana ndiyo haya inamfanya kipa wa upande wa pili kuonekana mbovu au kawahujumu wenzake.

YouTube player

Nilikuwa na mashaka sana na mporomoko wa ufungaji ndani ya Yanga si kwamba Mayele hafungi la hasha nilikuwa natizama ukame wa kucheza dk 270 yaani mechi tatu bila kufunga hata goli.

Niligusa kujisahau kwa makocha wengi baada ya kumaliza “pre season” huwa hawarudi mara kwa mara baadhi ya vitu vya kiufundi kama “finishing drills” nk.

Kwa aina ya magoli waliyofunga Yanga unaweza kuona wameyafanyia kazi kama timu na kukumbushana kupiga mbali mara kwa mara ikiwemo kuingiza tabia nyingine ya mashambulizi ya kushtukiza ambayo awali hawakuwa nayo.

Dickson Ambundo akimuacha mlinzi wa Dodoma Jiji.

Nimejiuliza maswali chungu mbovu juu ya kocha wa makipa wa Dodoma jiji ni nani na aina yake ya ufundishaji, kwanini uwezo wa mdogo wangu Mohammed Yusuph kupangua mipira (punching force )ikatue mbali ni mdogo kwanini kila siku anafungwa magoli ya jamii moja?

Goli la rafiki yake Mauya ambaye alikuwa wote Lipuli sitaki kusema wanafahamiana Ila nachoweza kusema Zawadi si mvivu kupiga hasa anapokuwa kwenye angle C ya uwanja anakumbuka kunyosha.

Kelvin John wakwanza kushoto, Mohamed Yusuph katikati na Tigana Lukinja wakiwa jukwaani Kasarani Kenya.

Mohammed Yusuph ni kipa wa timu ya Taifa katika wakati wa Ndyiragije na hapo pichani tulikuwa Moi kasarani Nairobi kwenye mmchezo wa kufuzu Chan tukiwa na Kelvin John golini alikuwa mwanaume Juma Kaseja.

Ndani ya miaka miwili unataka kuniambia ameisha kabisa? Je hatupaswi kumshukia kocha wake wa makipa?

Sambaza....