Blog

Kiungo wa Uganda awatamani Taifa Stars

Sambaza....

Kiungo mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ Farouk Miya amesema atajitoa kwa nguvu katika mchezo wa kundi L kuwania kufuzu kwenye fainali za Mataifa Afrika mwakani dhidi ya Tanzania.

Akizungumza mara baada ya mazoezi ya Leo asubuhi Miya katika uwanja wa Mandela, Miya amesema mchezo dhidi ya Tanzania ni Kama Dabi ya Afrika Mashariki hivyo kwa mchezaji yoyote ambaye anapata nafasi ni lazima ajitoe kuhakikisha anakuwa na mchezo mzuri.

“Kwanza Namshukuru Mungu ambaye ametuongoza kumaliza mazoezi vizuri, nina furaha kujiunga na wenzangu, tuna ari nzuri sana na morali ya kutosha kwa ajili ya mechi ya Jumamosi,”

“Mechi hii ni Kama mechi nyingine tuliyocheza na Cape Verde, lakini mechi hii ina umuhimu wake na ni kubwa, Tunatakiwa kuonesha nguvu na nitajitoa kwa nguvu zote, itakuwa ni Kama dhambi kupoteza nyumbani,” amesema.

Miya ambaye anakipiga katika timu ya HNK Gorica ya Croatia haya ni mazoezi yake ya kwanza baada pamoja na wenzake baada ya kuwasili Uganda siku ya Jumatano.

Kwa sasa Uganda Ndio ambao wanaongoza Kundi L wakiwa na alama 3 baada ya ushindi katika mchezo wa kwanza dhidi ya Cape Verde huku Wapinzani wao Tanzania wakitoka sare ya bao 1-1 na Lesotho Jijini Dar es Salaam.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x