Sambaza....

Klabu ya soka inayomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni “KMC” wana Kino Boys wametema cheche kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Coastal Union katika VPL utakaopigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaaam.

Kuelekea mchezo wa kesho dhidi Coastal, klabu ya soka ya KMC imesema inaendelea na kampeni yake ya kurudisha alama zote walizopoteza wakati wanaanza ligi.

Chanzo kilieleza ” Kmc inaendeleza kampeni yake ya kurudisha alama zake zote ilizopoteza wakati wa mzunguko wa kwanza iwe kwa sare ama kwa kupoteza. Jkt Tanzania na Ruvu Shooting tayari wameshazirudisha, Coastal Union tulitoka nao sare mkwakwani sasa anakuja Uhuru atazitoa point zetu tatu”

Katika hatua nyingine pia Kmc imeongezewa nguvu baada ya kurudi kwa wachezaji wake waliokua majeruhi na kupata vibali kutoka TFF.

“Charles Illafyia tayari leseni yake imetoka hivyo yupo tayari kutumika kuanzia mchezo wa kesho. Pia wachezaji wetu waliokua majeruhi tayari wamerejea. Elius Maguri, James Msuva na Emmanuel Mvuyekure wamepona majeraha na wapo tayari kwa mchezo wa kesho” Kiliongeza chanzo cha habari hii.

KMC ambayo inakamata nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Bara huku ikijikusanyia alama 31 na mchezaji wake Emmanuel Mvuyekure akiwa na mabao 6 katika chati ya ufungaji mabao. Kwa upande wa Coastal Union wao wapo nafasi ya 9 wakiwa na alama 25.

Sambaza....