Sambaza....

Kikosi cha Manispaa ya Kinondoni KMC Wana “Kino Boys” leo wameendelea na kampeni yao ya kurudisha alama zao walizopoteza mzunguko wa kwanza baada ya kuipiga klabu ya Coastal Union kutoka Tanga.

“Kino Boys” leo waliikaribisha Coastal Union kutoa Tanga katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaaam na kuipa kipigo cha maana kwa kuifunga jumla ya mabao matano kwa mawili.

Ally Ally

Alikua ni Charles Illamfia aliefungua karamu hiyo ya mabao katika dakika za mwanzo kabla ya Alli Msengi kuongeza bao la pili na kuipeleka KMC mapumziko wakiwa mbele kwa mabao mawili kwa sifuri.

Kilipindi cha pili kilianza kwa kasi na kupelekea kuongeza mabao matatu na kufikisha jumla ya mabao matano “mkono”. Emmanuel Mvuyekure aliongeza bao la tatu kabla ya Cliff Antony na Elias Maguri waliongia kipindi cha pili kufunga bao moja kila mmoja na kufikisha jumla ya mabao matano.

Ayoub Lyanga akipambana na Aron Lulambo

Licha ya kufunga mabao matano leo lakini KMC watajilaumu wenyewe kwa kukosa nafasi nyingi za wazi. Pamoja na Emmanuele Muyekure kukosa penati katika kipindi cha pili cha mchezo.

Coastal Union walipata mabao yao mawili ya kufutia machozi kupitia kwa Ayoub Lyanga aliyefunga mabao yote mawili katika kipindi vha pili cha mchezo huo. Ayoub Lyanga leo alionekana mwiba kwelilweli kwa walinzi wa KMC huku mara kadhaa akifanya majaribio yaliyomuweka katika wakati mgumu mlinda mlango Juma Kaseja.

Ayoub Lyanga akiokota mpira baada ya kumfunga Juma Kaseja (Aliekaa chini kushoto)

Kwa matokeo hayo sasa KMC inafikisha alama 34 wakicheza michezo wakiwa nafasi ya 3 na kuishusha Simba yenye alama 33 wakiwa na michezo 14 katika msimamo wa Ligi kuu Bara.

Coastal Union wao wanabaki na alama zao 25 huku wakishika nafasi ya kumi wakiwa wameshuka dimbani mara 22. Coastal Union sasa wanarudi Mkwakwani Tanga kuisubiri African Lyon ambao watamenyana siku ya Jumapili.

Sambaza....