England's Manager Roy Hodgson reacts after nearly spilling his water during the press conference at Wembley Stadium, London.
EPL

Kocha Roy Hodgson kuvunja rekodi hii Jumamosi.

Sambaza kwa marafiki....

Kocha Roy Hodgson atakuwa kocha mwenye umri mkubwa kama ataiongoza timu ya Crystal Palace kucheza na Leicester katika michuano ya ligi kuu soka England kwenye uwanja wa King Power mjini Leicester.

Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool ataivunja rekodi ya Kocha Robby Robson ambaye aliiweka mwaka 2004 wakati akiiongoza Newcastle United akiwa na umri wa miaka 71 na siku 191.

Hodgson atakuwa na umri wa miaka 71 na siku 199 siku ya kesho Jumamosi na kwa maana hiyo kama hatotimuliwa ama kuachia ngazi mwenyewe hadi siku ya mchezo atakuwa ndiye kocha mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kuiongoza timu ya soka inayoshiriki ligi kuu England.

Makocha wengine ambayo wanashika rekodi ya kuongoza timu za England wakiwa na umri mkubwa ni pamoja na Sir Alex Ferguson miaka 71 na siku 139, Neil Warnock miaka 70 na siku 4, Guus Hiddink miaka 69 na siku 188, Arsène Wenger miaka 68 na siku 258 na Dick Advocaat akiwa na umri wa miaka 68 na siku 6.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.